Wednesday, May 27, 2015

KIWANDA CHA SARUJI CHA SIMBA CEMENTI CHATOA MIFUKO 300 KWA UJENZI WA KITUO CHA AFYA, KISIMATUI

 Afisa uhusiano kiwanda cha Saruji cha Simba Cementi cha Tanga, Noor Mtanga, akitoa maelekezo kabla ya makabidhiano ya mifuko 300 ya saruji yenye thamani zaidi ya shilingi milioni 3,540,000 kwa kijiji cha Kisimatui kata ya Pongwe halmashauri ya jiji la Tanga kwa ujenzi wa kituo cha Afya

 Meneja biashara kiwanda cha Saruji cha Simba Cementi alievaa suti (kulia) akiangalia namna ambavyo maandalizi ya makabidhioano ya mifuko 300 ya Saruji kwa uongozi wa kata ya Pongwe ikiwa ni ujenzi wa kituo cha Afya kijiji cha Kisimatui. Makabidhiano yaliyofanyika kiwandani hapo, kushoto mbele ni Meneja Rasilimali watu i , Diana Malambuji ambapo nyuma ni Meneja uzalishaji , Benedict Lema


 Meneja biashara kiwanda cha Saruji cha Tanga   Simba Cement  cha Tanga , Mattheus Roos, akimkabidhi diwani kata ya Pongwe halmashauri ya jiji la  Tanga, Uzia Juma, mifuko ya saruji 300 yenye thamani zaidi ya shilingi milioni tatu laki tano kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya cha Kisimatui  na makabidhiano kufanyika viwanja vya kiwanda hicho jana.
 Meneja Usalama na Mazingira kiwanda cha Saruji cha Simba Cement, Leon Bredt, akimkabidhi mifuko 300 yenye thamani zaidi ya shilingi milioni tatu lakini tano, Diwani kata ya Pongwe halmashauri ya jiji la Tanga  , Uzia Juma, ikiwa ni msaada wa ujenzi wa kituo cha Afya kijiji cha Kisimatui  makabidhiano yaliyofanyika ndani ya kiwanda hicho jana.
 Afisa Uhusiano kiwanda cha Saruji cha Simba Cementi cha Tanga, Nour Mtanga, akimkabidhi Diwani  kata ya Pongwe halmashauri ya jiji la Tanga,  Uzia Juma, mifuko 300 yenye thamani zaidi ya shilingi milioni tatu laki tano ikiwa ni msaada wa ujenzi wa kituo cha Afya kijiji cha Kisimatui. Nyuma kushoto  ni Meneja wa Biashara, Mattheus Roos akishuhudia makabidhiano hayo jana.



Sherehe hizo za makabidhiano yalifana ambapo nao waandishi wa habari hawakuwa nyuma kwa kuchukua kila kinachofanyika.

No comments:

Post a Comment