Sunday, May 24, 2015

SOMA MAKUBWA YALIYOANDIKWA MAGAZETINI LEO,MAYA 24 TZ

Uchambuzi huu wa magazeti unaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu cha Candle Education Centre Tanga. Kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita na wanaojiendeleza kielimu. Wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 7727246

WEEK
MWANANCHI
Hatimaye Rais Jakaya Kikwete amemtaja mrithi wake baada ya kuwataka wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kumchagua mgombea urais anayekubalika ndani na nje ya chama hicho.
Kikwete alisema hayo jana wakati akifungua kikao cha Halmashauri Kuu kwenye ukumbi wa ofisi ya makao makuu ya chama hicho mjini hapa, unaojulikana kwa jina la White House.
Kauli hiyo imekuja wakati chama hicho kikiwa kwenye wakati mgumu kupata mgombea mpya baada ya Rais Kikwete kumaliza muda wake wa vipindi viwili vinavyokubalika kikatiba, huku kukiwa na ongezeko kubwa la nguvu ya upinzani.
Juzi, Kamati Kuu ya CCM iliwaachia huru makada wake sita waliotumikia adhabu ya miezi 17 ya kuzuiwa kujishughulisha na shughuli za uchaguzi baada ya kubainika kukiuka sheria za uchaguzi za chama hicho kutokana na kuanza kampeni mapema.
Miongoni mwa makada hao, wamo wanaopewa nafasi kubwa ya kupitishwa na chama hicho na ambao kambi zao zimekuwa zikipambana vikali na kuweka wasiwasi wa kuivuruga CCM.
Lakini Kikwete, ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho, alionekana kufahamu hali inayoendelea na alitumia muda huo kueleza jinsi ambavyo CCM imejidhatiti kupata mgombea urais kwa kuzingatia maslahi ya chama hicho na ya Watanzania, akisema wakati wa kudhani mtu yeyote anayeteuliwa na chama hicho atachaguliwa na wananchi umeshapita.
Rais Kikwete alisema kikao cha Halmashauri Kuu kina umuhimu wake kwa sababu kitaamua ushiriki wa CCM katika Uchaguzi Mkuu na kutoa ratiba ya uteuzi wa wagombea wa chama hicho.
Rais Kikwete alisema watu wote wanachama na wasio wanacham wanasubiri kwa hamu uamuzi wa vikao vya juu vya CCM.
“Watanzania wote bila kujali itikadi zao wanaitazamia na kuitumainia CCM kutoa uongozi ulio bora kwa nchi yetu. Hali hii inathibitisha uleusemi wa Baba wa Taifa kwamba Rais anaweza kutoka chama chochotelakini rais bora atatoka CCM,”.
Alisema CCM inatakiwa kutambua na kuzingatia uzito wa wosia huo wBaba wa Taifa na kuhakikisha kuwa unatekelezwa kwa ukamilifu wake.
“Asiyesikia la mkuu huvunjika guu. Vikao vya Kamati Kuu, HalmashauriKuu ya Taifa na Mkutano Mkuu wa Taifa, vina jukumu maalumu la kuongozna kusimamia mchakato wa uteuzi ndani ya chama,  utakaotuwezeshkupata wagombea wanaofaa,”alisema.
“Wenye kukidhi kiu na matarajio ya wanachama wa CCM na wananchi waJamuhuri ya Muungano wa Tanzania ni sisi. Lazima tupate wagombewanaochagulika, tunapowapeleka kwa wananchi ambao wengi wao siywanaCCM.”
MWANANCHI
Ni wabunge 68 tu, wakiwamo mawaziri 10, waliokuwa ndani ya ukumbi wa Bunge wakati chombo hicho cha kutunga sheria kikipitisha bajeti ya Wizara ya Kilimo na Chakula, lakini uongozi umesema “hakuna tatizo”.
Bunge la Jamhuri ya Muungano linatakiwa liwe na wabunge 357 iwapo kumetokea muujiza wakahudhuria wote.
Idadi hiyo ndogo ya wabunge kwenye kikao muhimu cha kupitisha bajeti imetia fora kwenye kikao cha 11 cha Bunge la 10 ambalo limetawaliwa na utoro katika mikutano yake ya mwisho kutokana na akili za watunga sheria hao kuwa majimboni.
Licha ya idadi hiyo ndogo, bajeti hiyo ilipitishwa kwa kutumia utaratibu wa “guillotine”, ambao wabunge hutakiwa na kiti cha Spika kutohoji jambo lolote katika vifungu mbalimbali vya bajeti husika anapoona havunji sheria.
Utaratibu huo hutumika wakati muda wa kawaida wa kikao husika au wa nyongeza unapomaliza huku utaratibu wa kupitisha vifungu ukiwa bado haujakamilika.
Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu ambaye aliongoza kikao cha jana asubuhi, alisema: “Bajeti za wizara zinaweza kupitishwa hata kama idadi ya wabunge ikiwa ndogo.  Katika bajeti kuu (wa wizara ya fedha) hapo ni lazima wabunge wote wawepo, akidi lazima izingatiwe.”
Kanuni ya 77 ya Bunge inayozungumzia akidi ya wabunge inayohitajika katika kikao cha Bunge kwa ajili ya kupitisha maamuzi, inaeleza kuwa lazima wawe zaidi ya nusu ya wabunge wote.
Hata hivyo, iwapo mbunge atasimama na kuomba muongozo wa Spika kama ataona ikidi ni ndogo, kiti cha spika kinaweza kutoa uamuzi wa wabunge wote kuhesabiwa na kisha kuwahoji wabunge kama wataridhia bajeti kupitishwa na idadi hiyo ama la. Jambo hilo halikutokea jana kwa sababu hakuna mbunge aliyehoji.
Mbunge wa Maswa Magharibi (Chadema), John Shibuda alisema kuwa jambo hilo si sawa na kinachofanyika ni “kufunika kombe mwanaharamu apite”.
“Ninachokiona ni mambo ya kuburuzwa tu. Yaani ili mradi tu bajeti imepita. Idadi inatakiwa kuwa nusu au kuzidi,” alisema mbunge huyo wa zamani wa CCM.
MWANANCHI
Wananchi wa Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma jana walikumbwa na taharuki baada ya askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuvamia mitaa, ofisi za Serikali na binafsi, benki, nyumba za ibada na katika maeneo ya biashara wakiwa na silaha huku magari yao yakiranda kila kona na kuanza kuwapekea watu wote waliyekutana naye huku wakidai kuonyeshwa vitambulisho.
Hata hivyo, hiyo ni mara ya kwanza kwa wanajeshi hao kuchukua hatua hiyo ambayo ilielezwa kuwa ni sehemu ya mazoezi na mafunzo kwa vitendo.
Wananchi waliohojiwa na gazeti hili kwa nyakati tofuti kufuatia kizaazaa hicho akiwamo Anastazia Mhale alisema alikutana na wanajeshi hao alipokuwa akielekea benki, walimsimamisha na kumuuliza maswali kisha wakamfanyia upekuzi.
“Nilishangaa kusimamishwa na wanajeshi na kutuhoji maswali huku wakitutaka tuwaonyeshe vitambulisho, hali hii iliwakuta hata watu waliokwenda wanakwenda sokoni,”Mhale.
Alisema mbali ya kuwakagua raia, pia walisimamisha kila gari barabarani na kulifanyia upekuzi sambamba na abiria waliokuwa ndani ya magari hayo.
Erasto Haule alisema: “Hata kama hakuna madhara yoyote wangetutangazia kama wanafanya mazoezi, wametutia hofu kubwa,” 
Alisema baadhi ya watu jana walishindwa kutoka kwenda kuendelea na shughuli zao wakihofi kukamatwa na wanajeshi hao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikhela alipoulizwa alisema zoezi hilo ni la kawaida na aliwataka wakazi mjini humo kuwa na amani na waendelee kufanya shughuli zao kama kawaida.
Gazeti hili pia liliwashuhudia askari hao wa jeshi wakiwa wametanda eneo lote la ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, lilipotaka kwenda kuonana na mkuu wa mkoa ili atolee maelezo zoezi hilo.
Alipoulizwa Brigedia Jenerali wa Kamandi ya Kusini, John Chacha alisema hiyo ni sehemu ya mafunzo kwa wanajeshi hao.
Alisema JWTZ hufanya mafunzo mbalimbali ya kujiimarisha ikiwamo ya kulinda miji, maporini na mengineyo.
MWANANCHI
Baraza la Madiwani la Manispaa ya Kinondoni limelazimika kupiga kura ili kupitisha mapendekezo ya kuyagawa majimbo ya uchaguzi kutoka matatu ya awali ili yawe matano kama ilivyopendekezwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Dalili za kutofautiana kwa wajumbe hao zilianza kuonekana tangu mwanzo wa kikao baada ya diwani kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) kupendekeza ipigwe kura ya maoni kama wasingekubaliana.
Majimbo yanayotakiwa kugawanywa ni Ubungo, Kawe na Kinondoni.
Kauli hiyo ilipingwa na wajumbe kutoka vyama vya upinzani wakiwamo Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika ambaye aliamua kutoka nje ya ukumbi kwa kile alichoeleza kuwa madiwani wa CCM walishafikia uamuzi kabla ya kuingia ukumbini.
Injinia Mussa Natty aliyataja majimbo mapya kuwa ni Kibamba na Mambwepande na kwamba, uamuzi huo umefikiwa kwa kuangalia kigezo cha idadi ya watu.
“Ukuaji wa miji unawafanya wakazi wengi kuhamia katika maeneo ya pembezoni kwa kasi katika kata za Kibamba, Goba, Bunju, Makubuli, Kimara, Mbweni, Kunduchi na Mbezi ambayo mwaka 2012 yalichukuliwa kuwa ni ya vijijini,” Injinia Natty.
Pia, alisema mapendekezo ya kugawa majimbo hayo yamezingatia mgawanyo wa huduma za kijamii na kiuchumi kama shule, masoko, huduma za afya na miundombinu ya barabara.
Kwa upande wake Mdee alisema NEC imekiuka utaratibu wa kugawa majimbo kwa kuwa Katiba inaitaka tume hiyo kufanya uchunguzi kwanza na kueleza sababu za kugawa majimbo jambo ambalo halijafanyika.
“Siogopi kugawanywa kwa majimbo kwa sababu tunapunguziwa mzigo, lakini nahoji kwanini katika kugawa majimbo baadhi ya kata zimechanganywa? mfano Kata ya Mwananyamala imewekwa Kawe halafu Kata ya Makumbusho ipo Kinondoni?”  Mdee.
Mstahiki Meya wa Kinondoni, Yusuph Mwenda alisema Manispaa ya Kinondoni ina watu milioni 1.8 kwa hiyo kila jimbo sasa litakuwa na takriban watu laki nne.
Baada ya kushindwa kufikia muafaka, Mwenda aliwataka wajumbe kupiga kura, ndipo 10 walinyoosha mikono kupinga uamuzi huo huku 20 wakipendekeza majimbo kugawanywa.
“Walio wengi wameshinda hivyo majimbo yatagawanywa,” alisema Mwenda.
NIPASHE
Mjumbe  wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na wakili mashuhuri nchini, Mabere Marando, ametangaza kujitoa mhanga katika uchaguzi mkuu wa Oktoba, mwaka huu kwa kutangaza matokeo ya uchaguzi kabla hayajachakachuliwa.
Marando ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Kanda ya Pwani, alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam wakati wa kongamano la mahafali ya vijana wa Chaso wanaotarajia kuhitimu vyuoni hivi karibuni.
Katika mkutano huo ambao Marando alitoa mada inayohusu Umoja wa Katiba  ya Wananchi (Ukawa) na nafasi ya vijana katika uchaguzi mkuu, alisema kuwa iwapo au isiwapo sheria  ya makosa ya kimtandao atajitosa kutangaza matokeo hayo usiku huo huo atakapoyapata na yupo tayari kupelekwa mahakamani.
“Nitatangaza matokeo kesho yake wakinipeleka Kisutu haya tu, wamezoea kukaa na matokeo siku tatu hadi nne, mimi sitangoja tena nitamwambia Dk. Slaa na Mbowe hili ninalofanya haliwahusu, serikali ikiamua kunipeleka mahakamani tutaangalia sheria inasemaje kwa sababu nitatangaza matokeo ya Chadema,”.
Alisema historia inaonyesha matokeo hasa ya Urais yamekuwa yakicheleweshwa makusudi.
Aliwataka vijana wa Chaso kuwa wajasiri kwani ndio watakaowezesha Ukawa kuchukua dola.
“Mbowe hataki kusikia tumeibiwa kura kwa sababu ya kuhesabiwa kwenye vituo vya kupigia kura, uchaguzi ulioisha mawakala wetu walikuwa wakichukua matokeo ya ubunge na kuondoka vituoni huku wakiacha ya urais,”.
Alisema mawakala wameelekezwa uchaguzi huu wachukue matokeo yote ya udiwani, ubunge na urais ili wizi utakapotokea iwe rahisi kuubaini.
“Uwezekano wa kushinda tunao sio tu ubunge bali urais, lakini hili litategemea uongozi na udhibiti,” alisema.
Alisema tofauti ya Ukawa na CCM kwenye uchaguzi mkuu, CCM inataka ushindi ili kurithisha watoto wao uongozi na kuendelea kutetea matumbo yao, wakati Ukawa lengo lao ni kutumikia wananchi.
Aidha, Marandu alitoa wito kwa Chaso mkoa wa Dar es Salaam wasikubali kurudi vijijini kabla ya kujiandikisha kwa sababu watakosa haki yao ya msingi.
“Tumebaini janja ya CCM wanataka wakati wanaandikisha Dar es Salaam nyie mtakuwa vijijini ambapo huko tayari zoezi limeshafanyika, fanyeni kila muwezalo mjiandikishe hapa,” .
Alisema wakati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alitaja adui watatu wa maendeleo kuwa ni ujinga, maradhi na umaskini na watawala wa sasa wameongeza ufisadi wa CCM.
Mjumbe wa Kamati Kuu wa chama hicho, Profesa Mwesiga Baregu, katika mada yake ya changamoto wanazokutana nazo wanachuo wenye fikra, aliwataka kuzilinda kura vituoni na kwenye kumbukumbu.
Alisema uchaguzi uliopita wapiga kura walipungua kwa asilimia 40 hivyo kuwahimiza vijana kuhamasishana kujiandikisha.
NIPASHE
Kanali mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Ameen Kashimir, ameilalamikia serikali kwa kutotambua mchango wake licha ya kuinusuru serikali wakati wa maasi ya jeshi hilo ya mwaka 1964.
Kadhalika, alisema pamoja na mchango wake kwa taifa mpaka sasa analipwa Sh. 22,000 kwa mwezi kama mafao ya uzeeni.
Kashimir ambaye alikuwa afisa wa kwanza kupata Kamisheni Jeshi la Tanganyika Rifles, kabla ya uhuru na baada ya uhuru, alikuwa Mnadhimu Mkuu wa kwanza wa jeshi hilo ambaye alifanya mambo mbalimbali ikiwemo kuwafundisha wanajeshi 30,000 kwa ajili ya kuanzisha jeshi jipya.
Hayo aliyasema jana jijini Dar es Salaam wakati alipohojiwa na waandishi wa habari wakati wa uwasilishwaji wa video kuhusiana na historia ya maisha yake.
Alisema mchango wake katika jeshi umesahaulika licha ya kwamba umesaidia kujenga msingi wa jeshi kutoka askari 50 waliobakia baada ya waasi na kuanzisha jeshi jipya la wanajeshi 30,000.
Alisema jeshi hilo lilikuwa imara na lilionyesha uhodari wake katika vita dhidi ya Idi Amini wa Uganda.
Kashmir alisema, yote waliyoyafanya yamesahaulika. “Kwa mimi binafsi nilibaki na cheo cha Kanali wakati nilitakiwa kuwa Meja Jenerali sasa hapa labda kulikuwa na ubaguzi wa aina fulani au sijui ni nini lakini nadhani serikali inatakiwa kuangalia suala la maofisa wa zamani.”
“Kwa mfano Jenerali Mstaafu Mrisho Sarakikya mafao anayopata ni Sh. 50,000 kwa mwezi na mimi napatiwa Sh. 22,000 na kama nisingekuwa na akili timamu na nguvu ningekuwa maskini na kuomba omba,” anasema.
Aliomba serikali ifikirie upya waliojitolea na kusaidia kujenga jeshi linaloonekana sasa wakumbukwe katika michango yao.
Aidha, alisema vijana wanatakiwa kuiga mfano wao kwa kuwa walikuwa ni wazalendo na nchi yao.
Alisema kuonyeshwa kwa video hiyo kutasaidia vijana kuelewa kazi walizokuwa wakizifanya  katika kujenga nchi.
NIPASHE
Watu wawili, mke na mume wakazi wa  Makambo, wilayani Mlele, wameuawa kikatili kwa kuchinjwa na kutenganishwa kichwa na kiwiliwili wakati wakiwa wamelala.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, aliwataja wanandoa hao  kuwa ni  Seth Mwakalimbwa (65) na Yakoba  Kalulu (48).
Kidavashari aliwaambia waandishi wa habari kuwa tukio hilo lilitokea Mei 21, usiku nyumbani kwa wanandoa hao ambao baada ya kuuawa miili yao iliachwa kitandani.
Alisema marehemu hao wakati wa uhai wao walikuwa wakiishi kwenye nyumba yao peke yao kwa muda mrefu.
Alisema,  balozi wa eneo hilo, Wilbroad Mahenge, ndiye aliyegundua vifo hivyo baada ya kutowaona wanandoa hao kwa siku mbili mfululizo na kuingiwa na wasiwasi.
NIPASHE
Kambi ya upinzani imesema migogoro ya ardhi baina ya wakulima, wafugaji na wawekezaji haiwezi kupatiwa ufumbuzi kutokana na baadhi ya watendaji waandamizi serikalini kuwa sehemu ya matatizo hayo.
Msemaji wa kambi rasmi ya upinzani katika Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Meshack Opulukwa, alisema Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), haina nia dhati kumaliza migogoro hiyo.
Alisema kutokana na hali hiyo, migogoro hiyo itaendelea kudumu kwa muda mrefu zaidi kwa sababu baadhi ya watendaji serikalini kuwa sehemu ya matatizo hayo.
Hali ya sasa ya migogoro hiyo ni mbaya zaidi na inatishia kutoweka kwa amani, umoja na utangamano wa wananchi katika maeneo yenye migogoro na taifa kwa ujumla.
Alisema katika maeneo yenye migogoro, uhasama baina ya wakulima, wafugaji, wawekezaji na watumiaji wengine wa ardhi umefikia kiwango cha juu.
Alisema hayo wakati akichangia hutuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2015/16 bungeni jana.
HABARILEO
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad, amebaini kuyeyuka kwa fedha za kodi Sh bilioni 835.974, katika mizigo iliyofika katika Bandari ya Dar es Salaam na kutakiwa kwenda katika nchi nyingine.
Kwa mujibu wa taarifa yake iliyotolewa bungeni wiki hii, ukaguzi wake katika mapitio ya mfumo wa kutunzia taarifa za forodha (Asycuda++), umebaini kuwa mizigo 6,316 iliyopaswa kufika katika Bandari ya Dar es Salaam kwa muda, haina ushahidi wa kuondolewa katika bandari hiyo.
Kwa kuwa hakuna ushahidi wa mizigo hiyo kuondoshwa kwenda katika nchi ilikokusudiwa, CAG amebainisha kuwa kama imeingizwa nchini, itakuwa imeikosesha Serikali kodi yenye thamani ya Sh bilioni 835.974.
Mizigo hiyo iliyoingizwa kwa muda, ina kodi ya jumla ya Sh 835,974,894,995. Mali na mitambo mingine, inayoingizwa nchini kwa muda, inaweza kutumika nchini kinyume na matakwa ya sheria hivyo kuikosesha Serikali mapato,”  Prof. Assad.
Kutokana na hali hiyo, Profesa Assad ameishauri Serikali kwa kupitia Mamlaka ya MapatoTanzania (TRA), kufanya uchunguzi juu ya bidhaa na vifaa vilivyoingizwa kwa muda kwa lengo la kukusanya kiasi cha kodi husika.
“Pia nashauri Serikali iweke udhibiti imara, utakaowezesha kusimamia maingizo yote ya muda na utakaohakikisha kuwa bidhaa hizo hazitumiki hapa nchini,” ameshauri Prof. Assad.
Wizi misamaha ya kodi CAG pia katika ukaguzi wake, alibaini wizi unaofanyika katika misamaha hiyo na kunufaisha watu binafsi, ambao wamekuwa wakiagiza vitu binafsi ikiwemo magari na kuyapitisha kwa jina la kampuni na asasi zenye misamaha ya kodi na baadaye kuirejesha.
Kwa wamiliki binafsi. Moja ya ufisadi wa aina hiyo, umekutwa katika Kampuni ya Kiliwarrior Expedition Ltd yenye msamaha wa kodi, ambayo iliagiza magari 28 bila kulipa kodi.
Unahitaji chochote kupenda kujua au kuabarika? usiwe mbali nami ni hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment