Thursday, May 28, 2015

MJANE WA MAREHEMU AVAA SHELA LA HARUSI AKIENDA KUMZIKA MUME WAKE

Huwezi kuamini kama huu ni msiba, mke wa marehemu akavalishwa na shela kabisa !!

Bibi harusi
Sio tukio la kawaida kukutana na mtu kavaa gauni la harusi kwenye mazishi..  Kenya kuna hii stori kutoka Kaunti ya Vihiga, unaambiwa mwanamke aliyefiwa na mume wake akalazimishwa kuvaa gauni ambalo anavaa bibi harusi wakati wa kufunga ndoa, alafu safari ya kwenda kwenye mazishi ikaanza.
Mary Akatsa ni kiongozi wa Kanisa la Jerusalem Church of Christ alikuwa akiongoza kila kitu mpaka mazishi yalipoisha,  mama alionekana a mkali hivi kama unaenda tofauti na maagizo yake.. wengine wanapigwa mpaka vibao.
Mazishi yalikuwa kama sherehe tu, kama ukiiona  video hiyo unaweza kuhisi labda watu walikuwa kwenye harusi au sherehe nyingine ya kawaida.

No comments:

Post a Comment