Haya ndio majina ya ‘mikorogo’ ambayo nimeijua leo baada ya Wabunge kuitaja Bungeni !!
Basi kama hukupata nafasi kuwa karibu na
TV au radio yako kufuatilia Bunge la leo MAY 28 2015 Dodoma, kwenye
maswali na majibu likawepo na hili linalohusu mkologo.. sikujua kabisa
kwamba kumbe hii mikorogo ya urembo ina majina kabisa mtu wangu !!
Swali la kwanza lilihusu Serikali imejipangaje kuzuia mikorogo iliyopewa jina la king’amuzi na mchiriku?
Jibu: “TFDA
imeandaa orodha yote ya vipodozi ambavyo havifai kwa matumizi ya
binadamu, wananchi wanatakiwa wasitumie vipodozi hivyo kwa kuwa vina
madhara.. mchiriku na ving’amuzi ni baadhi ya vipodozi visivyofaa kwa
binadamu ”>> Juma Nkamia.
Baada ya jibu hilo wakasimama Wabunge wenye maswali mengine hapahapa kwenye mikorogo: “Dini
zinakataza mwanadamu kujibadilisha, inavyoonekana Watanzania
hatujaridhika Mungu alivyotujaalia… Nikimwambia Waziri tutoke tuingine
barabarani atavikuta vipodozi visivyo na kiwango… Waziri anasemaje ili
kuhakikisha wanawake na wanaume anawanusuru matatizo haya?”>>> Mbunge Riziki Omar Juma.
Jibu: “Suala
la kuiga limekuwa kubwa sana, tunapoiga tuige mambo mazuri… TFDA
inafanya juhudi kukabiliana na vipodozi vinavyoingia nchini na havikidhi
kiwango.. vingi vimekuwa vikiteketezwa”>>> Juma Nkamia.
Likaja swali jingine: “Viongozi
wanatakiwa wame mfano ili raia wasifuate mtindo huu, Waziri anatuambia
nini ili suala hili lianzie na Wabunge wenzetu wanaojipodoa na kuvaa
nywele za bandia katika Bunge hili ili wawe mfano?” >>> Ibrahim Sanya.
Hili swali Naibu Spika Job Ndugai ikabidi alimalize juu kwa juu: “Hili swali sitaruhusu majibu, ni swali la uchokozi kwa Wabunge“
No comments:
Post a Comment