Saturday, May 30, 2015

DUBAI KUJENGA VIWANJA CHINI YA ARDHI

Dubai wamekuja na hii teknolojia ya uwanja chini ya bahari!!..(Pichaz)

dubaiii
Dubai ni moja kati ya miji inayokua kwa kasi sana duniani. Na ni miongoni mwa miji ambayo inafahamika kwa majengo ya kipekee na kifahari huku watu wengi kutoka sehemu mbali mbali duniani wakivutiwa kwenda Dubai kutalii ama kufanya biashara.
tee
Kwenye headlines leo ni mpango wa kuboresha michezo nchini humo, ambapo unaambiwa wameaamua kujenga uwanja wa kisasa wa mchezo tennis chini ya bahari.
Dubai wako kwenye mkakati wa kutekeleza project yao mpya unaojulikana Underwater Tennis Stadium itakayowezesha mashabiki wa mchezo wa tennis Dubai na duniani kuenjoy kucheza au kushuhudia mechi za tennis chini ya maji.
fish
Krzysztof Kotala ndio msanifu majengo mkuu anaehusika na ujenzi wa uwanja huo  wa chini ya maji na anasema anataka uwanja uwe zaidi ya uwanja wa michezo kwani utakuwa na sehemu ya vivutio vya kitalii kwa watu wanaopenda kwenda Dubai kwa matembezi yao binafsi.
dd
Kwa habari na matukio kemkem usiache kuwa mbali nami nitakuhabarishia na kukufikishia kila kitu hapa hapa tangekumekuchablog

No comments:

Post a Comment