Tangakumekuchablog
Tanga, DIWANI
viti maalumu (CCM) kata ya Chumbageni
Tanga, Saida Gaddaf, amewataka vijana kuunda vikundi vya Ujasiriamali ili
kuweza kupata fursa za mikopo pamoja na asilima tano ya halmashauri ya jiji
iliyotengwa kwa vijana.
Akizungumza wakati wa makabidhiano
ya pikipiki 15 zilizotolewa na kampuni ya Fecon kwa Umoja wa madereva wa
pikipiki na bajaj (Moperoo Investment) jana Gaddaf, aliwataka vijana kuunda
vikundi kuchangamkia fursa za mikopo.
Aliwataka vijana kuacha kubweteka
wakati fursa ziko nyingi za kujiletea maendeleo na kuweza kupata asilimia tano
zilizotengwa na halmashauri kwa ajili ya vijana.
“Najisikia fahari kuona vijana
mumeunda umoja ambao ni mfano wa kuigwa
na kuweza kuaminiwa kwa kupewa pikipiki----hii ni fahari kwa wakazi wa kata
yangu na ni fahari kwa wakazi wa Tanga”
alisema Gaddaf na kuongeza
“Kupitia hafla hii fupi ya
makabidhiano niwambie vijana kuchangamkia fursa za mikopo kwenye taasisi za
fedha pamoja na asilimia tano iliyotengwa kwa ajili ya vijana” alisema
Diwani huyo alitoa wito kwa vijana
kuacha kujikalia vijiweni na kupiga soga jambo ambalo linaweza kuzalisha
matukio mabaya yakiwemo ya uporaji na uvutaji wa bangi na hivyo Taifa kupoteza
nguvu kazi.
Kwa upande wake, Afisa masoko
kampuni ya Pikipiki (Fecon) ,Zakayo Liang, ameutaka umoja huo kuweka sheria
nafuu za vijana ambao wanataka kujiunga
ili kuweza kupata fursa za kujikwamua na maisha.
Alisema kuwepo kwa sheria nafuu
kutawawezesha vijana wengi kujiunga na vikundi vya ujasiriamali na kuweza
kujikwamua na maisha jambo amblo litawawezesha pia kuepukana na magenge ya
kihuni.
“Niweze kuwashauri ndani ya umoja
wenu kuweka sheria nafuu zitakazomvutia kijana kujiunga----hii itapelekea
kuondosha wimbi la vijana wasio na kazi” aliema Liang
Aliwataka kudumisha umoja na
mshikamano ili kuweza kuwa chachu ya maendeleo na mfano kwa wengine ikiwa na
lengo la kumkomboa kijana kutoka katika umasikini.
Diwani kata ya Chumbageni Tanga , Telesphory Chambo (CCM) akipokea pikipiki 15 kutoka kwa Afisa masoko kampuni ya pikipiki aina ya Fecon, Zakayo Liang zilizotolewa kwa Umoja wa Madereva wa pikipiki na bajaj (Moperoo Investment) zikiwa na lengo la kukopeshana ili kujikwamua na umasikini. Kushoto ni Diwani viti maalumu kata ya Chumbageni, Saida Gaddaf (CCM) na katikati ni Mwenyekiti wa Moperoo, Silas Stivin. | |||
Afisa Masoko kampuni ya pikipiki (Fecon), Zakayo Liang (kulia) akimkabidhi pikipiki 15, Afisa Maendeleo ya Vijana, Enersest Shekibua kwa niaba ya Umoja wa madereva wa pikipiki na bajaj (Moperoo Investment) ya mjini Tanga na makabidhiano kufanyika katika viwanja vya umoja huo jana.
No comments:
Post a Comment