Wednesday, May 27, 2015

ASTAGHFIRU LLLLAH, LAANA ZA WALIMWENGU

Unyanyasaji huu wa mama kwa mtoto wake kwenye headlines tena.

law
Matukio ya unyanyasaji kwa watoto yameendelea kuchukua headlines kila kukicha sehemu mbalimbali duniani.
Miongoni mwa matukio yaliyosikika siku za hivi karibuni ni pamoja na lile la mfanyakazi wa ndani kumtesa mtoto kule Uganda, na kule India kuna lile la mtoto wa siku nne kulazimishwa kutembea na mganga kwa madai atapona..Yote haya ni matukio ya unyanyasaji kwa watoto.
mtoto
Hili lingine limetokea hujo Ufilipono baada ya mama kuamua kumfunga mtoto wake mnyoyoro na kumwekea chakula kama mbwa kwa madai amekua akimsumbua.
mtoto2
Mama huyo aliweka picha za mwanaye huyo wa kiume akiwa uchi kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook, lakini picha hizo zilichukuliwa na wanaharakati wa haki za binadamu na kumfungulia mama yake mashtaka.
mtoto3
Mmoja wa wanaharakati hao  Lurleen Hilliard.  alisema kwa sasa mtoto huyo atakua chini ya kituo cha kulelea watoto wakati mama yake akitumia adhabu kwa unyanyasaji alioufanya.

No comments:

Post a Comment