Tuesday, May 26, 2015

WASAFIRISHA MAITI YENYE EBOLA KWA KUTUMIA STAIL MPYA

Watu sita wawekwa karantini jela Guinea

Watu sita wamewekwa karantini gerezani nchini Guinea baada ya kushutumiwa kusafiri wakiwa na mwili wa mtu aliyekufa kwa ugonjwa wa Ebola.
Mamlaka zinasema mwili huo ulikalishwa wima kwenye Taxi mithili mtu aliye hai, ukiwa umevaa T-shirt na Suruali aina ya Jeans na miwani ya jua akiwa kati kati ya Watu wengine wawili.
Guinea iko kwenye Kampeni ya kutokomeza ugonjwa wa Ebola.
Takriban watu 2,500 wamepoteza maisha nchini Guinea tangu ugonjwa huo ulipokumba Afrika Magharibi zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

No comments:

Post a Comment