Ishu ya ndoa za jinsia moja imechukua headlines tena, Ireland wameamua kupiga kura leo !!
Mwaka
1993 nchi ya Ireland ilikuwa moja ya mwisho mwisho kabisa katika nchi
za Ulaya kuhalalisha ishu ya uhusiano wa jinsia moja.. mpaka leo ni
miaka 22 imepita, wakati wowote huenda kukatokea headline nyingine
kuhusu suala hilo, Bunge liliamua hii ishu washirikishwe watu wao pia na
mpaka kesho Jumamosi May 23 2015 tutasikia nini kimepitishwa.
Watu wa Ireland wanaendelea kupiga kura
leo, kama kura nyingi zikisema YES, basi Katiba ya nchi hiyo itafanyiwa
mabadiliko na ishu ya ndoa za watu wenye uhusiano wa jinsia moja
zitakuwa zimeruhusiwa rasmi kwenye nchi hiyo !!
Kuna vitu vingi vinaendelea Ulaya, Marekani
na nchi nyingine ikiwemo hii ya kuhalalisha ndoa na uhusiano wa jinsia
moja, kwa Afrika ni nchi chache zimetoa msimamo.. Uganda ni moja ya nchi
ambazo zilikataa kuhalalisha ndoa za aina hiyo.
Kampeni zimeendelea mtaani, migahawani kuna mabango yaliyoandikwa “YES EQUALITY” kuonesha watu kwamba wapo watu ambao wako tayari kuyakubali mabadiliko hayo.
Usiwe mbali nami kila peruz kwa kupata habari matukio na michezo , ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment