Friday, May 29, 2015

UJUMBE WA CHRIS BROWN KWA WASHABIKI WAKE

Ujumbe wa Chris Brown: Unadhani umaarufu na pesa umemfanya awe hivi alivyo?

chrrr
Chris Brown ni mmoja kati ya mastaa wanaokubalika sana katika industry ya muziki wa R&B na Pop Music, duniani toka akiwa na miaka 16 na amekua mtu wa kuzungumziwa sana hasa katika mitandao ya kijamii kutokana na kuwa na skendo nyingi ndani na nje ya kazi yake.
Akiwa ni baba wa mtoto mmoja, jana alichukua muda na kuangalia maisha yake ya nyuma, ikiwemo makosa aliofanya, watu aliowaumiza na kumfanya kuandika ujumbe kwa mashabiki wake wa Instagram kuhusu mikasa yake ya kimapenzi, umaarufu na hela, na jinsi gani hivi vitu hivyo vimemuathiri yeye kama binadamu miaka michache iliopita mpaka sasa.
Chris Brown aliandika kuwa anashindwa kuelewa maisha yake yanakwenda wapi licha ya umaarufu alionao, na amekuwa akijikuta anawaumiza sana watu hasa waliokaribu nae kwani kuna kipindi kilifika akawa hajitambui yeye ni nani, lakini sasa hivi amekua akiongea sana na Mungu na amejifunza kuishi na mapungufu yake kwa sababu anaamini hakuna aliyekamilika.
Pesa, umaarufu na kushindwa kumudu mahusiano yake ya kimapenzi kwa watu waliokuwa wakimjali umemfanya awe jinsi alivyo na kuonekana mbaya mbele za watu.
Kutana na ujumbe wake wa Instagram hapa chini mtu wangu:
image
Kwa habari matukio na michezo, tembelea blog hii kila wakati itakupa kila kinachotekea ndani na nje ya nchi hapo hapo

No comments:

Post a Comment