China yatakiwa kusitisha ujenzi baharini
Marekani imetaka kuwepo usitishwaji wa ujenzi wa miradi kwenye maeneo yanagombaniwa katika bahari ya kusini mwa China.
Waziri
wa ulinzi wa Marekani Ash Carter aliuambia mkutano mkuu wa ulinzi
nchini Singapore kuwa tabia ya China eneo hili imekiuka sheria za
kimataifaCarter amesema kuwa kuvihami kijeshi visiwa bandia ambavyo vinajengwa na China ni hatua inayoweza kusababisha mizozo ya kijeshi.
Matamshi yake yamekuja siku moja baada ya makao makuu ya jeshi la marekani kusema kuwa china imeweka silaha katika moja ya visiwa hivyo.
Carter anasema kuwa hakutakuwa na suluhu la kijeshi . Hata hivyo amesema kuwa Marekani itaendelea kuwa na jeshi lake katika eneo hilo.
Hutopitwa na habari inayonifikia na nitakusogezea kila kinachonifikia hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment