Tangakumekuchablog
Tanga,KIWANDA
cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga, kimetoa mifuko 300 ya saruji kwa ajili
ya ujenzi wa kituo cha afya kijiji cha
Kisimatui ili kuondosha kero ya kufuata matibabu masafa marefu kwa wakazi wa
eneo hilo na vijiji vya jirani.
Akizungumza wakati wa halfa fupi ya
makabidhiano juzi, Meneja Biashara kiwanda cha Saruji cha Simba Cement,
Mattheus Roos, alisema msaada huo umekuja baada ya maombi ya wakazi wa kijiji
cha Kisimatui na maeneo jirani kwa muda mferu wamekuwa wakifuata matibabu masafa
marefu.
Alisema kufuatia kero hiyo kiwanda
cha saruiji kiliguswa na kuona ili kuweza kupatikana kito cha afya ni vyema
kutoa mifuko 300 ya saruji na kuikabidhi kwa viongozi wa kijiji kwa kuanza
ufyatuaji wa matofali.
“Kiwanda cha saruji imetoa mifuko
mia tatu yenye thamani zaidi shilingi milioni tatu na laki tano-----ni sera ya
kiwanda kusaidia jamii ikiwemo elimu na mazingira” alisema Roos na kuongeza
“Kiwanda itahakikisha kituo
kinajengwa haraka na kukamilika kama ilivyopangwa na tutakuwa bega kwa bega na wananchi
-----ni imani yetu kituo hiki kitakuwa msaada pia kwa vijiji vya jirani”
alisema
Kwa upande wake diwani kata ya
Pongwe (CCM), Uzia Juma, alisema msaada huo utatumika kama ulivyopangwa na
kuyataka makampuni mengine kuiga ili kuweza kukamilisha ujenzi wa kituo cha
afya.
Alisema kwa muda mrefu wakazi wa vijiji
vya Kisimatui, Pongwe na Kichangani wamekuwa katika wakati mgumu wa kupata
matibabu na badala yake wamekuwa wakisafiri masafa marefu.
“Kwa miaka mingi wakazi wa Kisimatui
na vijiji vya jirani wamekuwa wakifuata matibabu umbali zaidi ya kilometa
kumi---- ujio wa kituo hiki itakuwa mkombozi kwa wengi na asanteni kiwanda cha saruji”
alisema Juma
Aliwataka wananchi na viongozi wa
kijiji cha Kisimatui kushirikiana kuwezesha
kujengwa kwa kituo hicho na kutaka kutumiliwa kwa saruji hiyo kama ilivyopangwa.
Mwisho
No comments:
Post a Comment