Monday, May 25, 2015

UVAAJI NGUO FUPI CHINA DILI

Kama ukivaa nguo fupi kuna ofa yako kwenye mgahawa huu China…

gllll
Hapa kwetu wanawake wanaovaa nguo fupi wanakua katika wakati mgumu sana wanapopita barabarani licha ya kuwa ni moja ya mavazi ya kisasa ambayo wanawake wengi wamekuwa wakivaa.
Kwa nchi za wenzetu si jambo la ajabu kuona wanawake wakiwa ndani ya mavazi mafupi na kutembea bila wasiwasi barabarani, mna leo kuna hii ya uvaaji wa nguo fupi iliyotokea China.
Kuna mgahawa mmoja China umejitolea kuwapa punguzo wanawake wote watakaokuwa wakivaa nguo fupi wanapoingia ndani ya Mgawaha huo.
Wahudumu wa Mgahawa huo wamepewa kazi ya kupima ufupi wa nguo zitakazovaliwa na wanawake wote wanaokwenda hapo na unaambiwa kumekuwa na foleni ya wanawake wanaoingia hapo ili kupata punguzo hilo kila wakati.
Punguzo hilo huanzia asilimia 20 hadi 90 ya gharama ya chakula na vinywaji na hutegemea na jinsi muhusika alivyovaa.
Yang Jia Hot Pot ambaye ni meneja wa mgahawa huo amesema baada ya kutoa ofa hiyo wamekuwa wakipata idadi kubwa ya wateja ambao wameongeza mauzo kwa kiasi kikubwa.

No comments:

Post a Comment