Sunday, May 31, 2015

BOKO HARAMU LAUWA WATU 29

Nigeria:Watu 29 wauawa msikitini

Watu 29 wameuawa katikati ya  mji mkuu wa jimbo la Borno Maiduguri Kaskazini Mashariki mwa Nigeria baada ya mlipuaji wa kujitoa mhanga kujilipua ndani ya msikiti.
Kamishna wa polisi katika jimbo la Borno amesema kuwa watu wengine 28 walijeruhiwa kwenye shambulizi hilo.
Shambulizi hilo lilifuatia jaribio la awali la kuuteka ya mji wa Maiduguri lililondeshwa na wanamgambo  wa Boko Haram.
Wanagamabo hao walifyatua makombora kwenye makazi ya watu na kuua takriban watu 13.

No comments:

Post a Comment