Saturday, May 23, 2015

USHETWANI

Ireland yaamua kuhusu ndoa za jinsia moja




Wapiga kura wengi wameripotiwa kujitokeza kwenye kura ya maoni nchini Ireland ya kuamua iwapo ndoa za watu wa jinsia moja zinaweza kuhalalishwa .
Katika sehemu nyingine ukiwemo mji mkuu Dublin na miji mingine, idadi ya wapiga ilitarajiwa kufikia takriban asilimia 60.

Ndoa za jinsia moja
Wataalamu wengi wa Ireland walio katika mataifa ya kigeni walirudi nyumbani kupiga kura.
Wale wanaounga mkono ndoa za jinsia moja walitarajia watu wengi kujitokeza.

Wapenzi wa jinsia moja wakitoka katika kituo cha kupiga kura
Ikiwa kura hiyo itafanikiwa Ireland itakuwa nchi ya kwanza kuhalalisha ndoa za jinsia moja kupitia upigaji kura.
Matokeo yanatarajiwa kutangazwa baadaye leo.
Usiache kupitia tangakumekuchablog kukuhabarisha juu ya matokeo ambayo yanatarajiwa kutangazwa mapema kuanzia muda huu

No comments:

Post a Comment