Friday, May 29, 2015

KITISHO CHA NJAA SUDANI KUSINI

Watoto elfu 250 huenda wakafa kwa njaa Sudan

Mshirikishi mkuu wa shirika la Umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini, Toby Lanzer, amesema kuwa takriban watoto laki mbili na  nusu wamo katika hatari ya kufa katika kipindi cha miezi kadhaa ijayo iwapo mashirika ya utoaji misaada, hayatafikisha misaada kwa watu walio na mahitaji.
 
 Lanzer ameiambia BBC kuwa, watu wanateseka kwa sababu ya umaskini.
Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan Kusini imesambaratisha uchumi wa taifa hilo.
Amesema kwamba mashirika ya utoaji misaada yatafanya yawezavyo kuwasaidia wahitaji, ikiwa  amani itapatikana tu nchini Sudan Kusini iwapo viongozi watakubaliana kukomesha mapigano.
Kwa habari na matukio mbalimbali yanayojiri usiache kuperus blog hii itakuhabarisha kila jambo muda na wakati muafaq

No comments:

Post a Comment