Saturday, May 23, 2015

MJI WA RAMADI WAKIMBIWA

Watu 40,000 waukimbia mji wa Ramadi

Mratibu wa huduma za kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq amesema kuwa huenda takriban watu 40,000 wameukimbia mji wa Ramadi ambao ulitekwa na wanamgambo wa islamic state karibu wiki moja iliyopita.
Dominik Bartsch aliiambia BBC kuwa watu wengi waliokimbia makwao wakiwemo watoto, watu wazee na wagonjwa wamekwama kwenye daraja moja linaloingia mjini Baghdad bbada ya kuzuiwa kuingia mji huo.
Anasema kuwa kuna ripoti kwamba baadhi ya watoto wameaga dunia baada ya kuishiwa na maji mwilini.
 Bartsch pia anasema kuwa Umoja wa Mataifa una wasi wasi kuhusu hatma ya wakimbizi waliojikuta kati kati ya mapigano kati ya wanamgambo wa Islamic State na vikosi vya Serikali.

No comments:

Post a Comment