Thursday, May 21, 2015

MKURUNZINZA UWANJANI, BUNJUBURA

Kingine kilichoripotiwa kutoka Burundi..Ni hii ya Rais Nkurunziza Uwanjani (Pichaz)

nziza2
Burundi kwa sasa ndiyo nchi inayozungumzia sana kutokana na vita ya kisiasa inayoendelea tangu Rais wake Pierre Nkurunziza atangaze uamuzi wake wa kutaka kuwania Urais kwa awamu ya tatu mfululizo.
nziza
Jaribio la kutaka kumpindua madarakani wakati akiwa Tanzania kwenye mkutano wa usuluhishi pamoja na Marais wengine wanaounga Jumuiya ya Afrika Mashariki, halikufanikiwa na sasa uamuzi uliofikiwa ni kuahirishwa kwa uchaguzi wa Wabunge ili kuzunguzia mustakabali mzima unaoendelea nchini humo.
pier
Stori mpya iliyotufikia leo ni kwamba pamoja na machafuko yanayoendelea nchini humo Rais huyo ameonekana kutojali na kuna picha ambazo zimesambaa kwenye mitandao zikimuonyesha akiwa uwanjani na wenzake akicheza mpira huku akionekana mwenye furahanziza3
Imeelezwa kuwa leo mtu mmoja amepigwa risasi ya mgongoni na askari wanaolinda usalama katika mji wa Bujumbura wakati wakiandamana katika ngome inayosadikiwa ni ya wapinzani.nziza4
Matukio , vimbwanga na burudani unazipata hapa kupitia tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment