Tuesday, May 26, 2015

URUSI YAFANYA MAZOEZI MKALI YA KIJESHI

Urusi yaanzisha mazoezi ya Kijeshi

Rais wa Urusi Vladimir Putin
Urusi imeanza mazoezi makali ya kivita yanayojumuisha kikosi cha anga cha wanajeshi 150 pamoja na kikosi cha mashambulio ya mbali ya makombora.
Wizara ya mambo ya ndani ya Urusi inasema kuwa wanajeshi 12,000 wanatarajiwa kuhusishwa na mazoezi hayo makali ya siku nne yanayolenga kutaka kujua uimara wa jeshi hilo na utayari wake.
Mazoezi hayo makali yanakuja sawa na yale yanayoendeshwa na vikosi vya NATO na majeshi ya Ulaya Nordic yanayojumuisha zaidi ya wapiganaji 100 wa jeshi la anga.
Hata hivyo tukio hili la mazoezi ya majeshi ya Urusi yanaleta kwa nchi za magharibi kufuatia machafuko yanayoendelea Ukraine ambapo Urusi imekuwa ikinyooshewa kidole kutokana na machafuko hayo.

No comments:

Post a Comment