Tuesday, May 26, 2015

EAC KUKUTANA TENA DAR ES SALAAM

Nchi za EAC kukutana mwishoni mwa Juma

Wizara ya Mambo ya nje Tanzania imetoa taarifa juu ya kuwepo kwa mkutano wa Viongozi wa Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam siku ya Jumapili ili kuangalia kwa mara nyingine tena hali ya amani nchini Burundi.
Jaribio la mapinduzi la kijeshi lililofanyika Mei 13 wakati Rais Pierre Nkurunziza akiwa nje ya nchi katika mkutano wa maraisi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ulifeli,na Rais kulazimika kurejea Burundi.
Mkutano huu unaotarajiwa kufanyika karibuni haujaweka wazi kama Raisi huyo wa Burundi atakuwepo ila umeweka bayana kuwa Burundi itawakilishwa vyema.
Upinzani nao nchini humo umegoma kufanya mazungumzo baada ya mmoja wa viongozi wake kuuwawa siku ya Jumamosi.
Machafuko ya sasa yamesababisha zaidi ya Raia 100,000 wa Burundi kukimbilia nchi za jirani Rwanda, Tanzania na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo

No comments:

Post a Comment