Sunday, May 24, 2015

ADONDOSHA MENO YOTE AKISHEREHEKA MIAKA YAKE 102 YA KUZALIWA

Mishumaa ya Birthday ikamtoa machozi bibi, kisa kaangusha meno yake..!!

bibi
Inawezekana kuonekana ni kichekesho lakini ni kweli imetokea baada ya bibi Louise Bonito kujikuta anaangua kilio katika sherehe ya siku yake ya kuzaliwa huko Australia.
Bonito ambaye ni bibi wa miaka 102 anayeishi katika mji wa North Haven alijikuta akipoteza meno yake yote ya mbele wakati alipokuwa akizima mishumaa iliyokuwa juu ya keki aliyoandaliwa na familia yake.
102
Louise Bonito akiwa na baadhi ya wana familia
Akiwa katika harakati za kupuliza mishumaa alishngaa kuona meno yake ya mbele yakidondoka  na kubaki kibogoyo.
Baada ya tukio hilo ilimlazimu  kuacha zoezi hilo na kuanza kulia jambo lililowahuzunisha wanafamilia, lakini wengine walikuwa wakiangua vicheko kutokana na tukio hilo.
K wa habari na matukio ndani na nje ya nchi ni hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment