Kumbe bangi kwa wengine ni dawa wengine ni chakula, iruhusiwe TZ?? Maswali na majibu toka Bungeni Dodoma !!>>
Kikao Cha Bunge kimeendelea leo MAY 26
2015 Dodoma, ukaibuka mjadala kuhusu Bangi.. Kuna nchi zimehalalisha
bangi kwa matumizi ya tiba na chakula, swali la kwanza lilikuwa la
Mbunge Cristowaja Mtinda aliyetaka kujua msimamo wa Serikali kwenye hili.
“Matumizi
ya bangi husababisha madhara mbalimbali ikiwa ni pamoja na
kuchanganyikiwa, ukatili, ukorofi.. Baadhi ya sehemu Duniani hutumia
bangi kama Chakula au dawa. Msimamo wa Sheria ya Tanzania inafuata
Sheria ambayo inaeleza kuwa mtu yoyote atakayejihusisha na kutumia,
kuhamasisha matumizi, kusafirisha ni kosa la jinai”>>>
Swali jingine; >>>“ Katika
nchi yetu kuna mikoa ambayo bangi huota bila kupandwa, mfano Njombe na
Iringa, wanaitumia kama chakula, Serikali imefanya utafiti gani kuona
faida za kimatibabu zinazoweza kupatikana kutokana na bangi ili itumike
kama dawa”>>>
Swali lake kwenye sentensi nyingine >>> “Kuna imani kwamba bangi huongeza nguvu, Serikali inatoa elimu gani kwa hao wanaotumia kwa imani ya kuongeza nguvu?“>>> Cristowaja Mtinda.
Jibu >>> “Bangi
inaota bila kupandwa lakini inang’olewa na watu… Bangi ni haramu
inafanya mtu achanganyikiwe na sidhani kama Serikali inaweza kuruhusu
itumike.. umezungumzia kwamba bangi inaongeza nguvu sijui ni nguvu zipi
za kike au za kiume”>>> Juma Nkamia.
Spika Anne Makinda akafunga hivi mjadala>>> “Tunaendelea… habari za bangi tuachane nazo”>>>
No comments:
Post a Comment