Thursday, May 28, 2015

DI MARIA ATAKIWA BAYERN MUNICH

Bayern Munich nayo yajitosa kunasa saini ya Di Maria…

diiii

Klabu za ligi kuu ya England zipo katika maandalizi ya msimu ujao wa ligi kuu huku baadhi ya klabu zikianza mchakato wa kusajili wachezaji wapya kwa ajili ya kutumikia klabu zao.
Wakati winga wa Manchester United Angel Di Maria akiendelea kuwa gumzo kutokana na dalili za klabu yake ya Manchester kutaka kumtema, Bayern Munich imeanza mikakati ya kutaka kumsajili ili aitumikie msimu ujao.
Di Maria bado ana mkataba na klabu yake ya Manchester na huenda klabu hiyo ikamtoa kwa mkopo kwenda kucheza kwenye klabu yoyote inayomtaka huku ikitoa sharti kuwa klabu yoyote inayomuhitaji inatakiwa kumlipia ada ya pauni milioni 59.7 ili kuweza kumpata.
Bayern imesema ipo tayari kutoa ofa kubwa zaidi ya iliyotangazwa na Paris St Germain ambayo nayo imepania kumnyakua winga huyo raia wa Argentina.
Kwa habari na matukio motomoto, usiwe mbali nami ni hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment