FIFA kwenye tuhuma za rushwa, kuna hawa maafisa wana kesi ya kujibu…
Wakati uchaguzi mkuu wa Shirikisho la soka dunia FIFA ukitarajiwa kufanyika keshokutwa, leo kuna taarifa mpya kutoka ndani ya shirikisho hilo.
Kumekuwa
na malalamiko mengi kutoka kwa mashabiki wa soka duniani ambao wamekuwa
wakilalamikia utendaji mbovu wa viongozi walioko madarakani na hadi
kupelekea wagombea waliokuwa wakiwania nafasi ya Urais ndani ya
Shirikisho hilo kuamua kujindoa.
Taarifa
mpya zinadai kukamatwa kwa tuhuma za rushwa kwa maafisa sita wa
Shirikisho hilo wakiwa katika hoteli moja ya kifahari mjini Zurich, Switzerland.
Maafisa hao ni pamoja na makamu wa Rais wa FIFA, Jeffrey Webb
na wanashikiliwa wakisubiri kupelekwa Marekani kwa ajili ya uchunguzi
huku Rais Blatter naye akiwa mmoja wa washtakiwa wlaiokuwa wakichunguzwa
kwa muda mrefu lakini hayupo kwenye orodha ya waliokamatwa.
Shutuma
hizo zinahusisha rushwa ya kiasi cha dola milioni 150 kwa kipindi cha
miaka 20 ambazo zilikuwa zikichunguzwa na wapepelezi kutoka Marekani.
Wanachama wa Fifa watakutana mjini Zurich kwa ajili ya mkutano wao wa mwaka siku ya ijumaa wakati rais wa Shirikisho hilo Sepp Blatter akiwa anawania nafasi hiyo kwa muhula wa tano akiwa amebaki peke yake.
Kwa matukio na habari usiwe mbali nami ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment