Tangakumekuchablog
Tanga,JAMII
imetakiwa kuwa na ada ya kupima afya zao ili
kuweza kujitambua na kutakiwa
kuacha kuficha magonjwa jambo ambalo linaweza kupunguza nguvu kazi ya Taifa.
Akizungumza wakati wa upimaji afya
na uchangiaji damu salama zoezi lililoendeshwa na Mfuko wa Afya jamii (NSSF),
Mratibu wa Udhibiti wa magonjwa ya Ukimwi Tanga, Suleiman Hassan, alisema watu
wengi hawana ada ya kupima afya zao.
Alisema hali hiyo imekuwa ikichangia
kushuka kwa kiwango cha uzalishaji mali baada ya watu wengi kuugua majumbani na
kuogopa kupima afya zao katika vituo vya afya.
“Tuseme ukweli kuwa hatuna ada ya
kujua afya zatu na badala yake tunapoteza nguvu kazi kwa kuugulia maradhi
ndani ya miili yetu----hebu tuthubutu jamni kutambua afya zetu sio dhambi” alisema
Hassan
“Utamkuta mtu anaugua malaria au
magonjwa ya tumbo wakati hospitali zimemzunguka hata ile kusema japo kipimo
kimoja ngoja niendele mtu hataki anataka kufa na tai shingoni” alisema
Aliitaka jamii kubadilika kwa kuwa
na ada ya kuhudhuria vituo vya afya kwa kupima ili kutambua magonjwa mtu
yanayomsibu na kuacha kuugulia maradhi kitandani jambo ambalo linaweza mtu
kukaribisha mauti.
Kwa upande wake, Meneja wa Bima ya
Afya Tanga, Ali Mtulya, amesema watu wengi wanaopata magonjwa ya shinikizo la
damu na presha ni kutokana na kutofanya mazoezi na kula vyakula bila mpangilio.
Alisema kula bila npangilio na
kuacha kufanya mazoezi kunamfanya mtu kupata magonjwa na hivyo kuwataka kuwa na
ada ya kupima afya zao na kufuata maelekezo
ya wataalamu wa tiba.
“Watu wengi wanaacha kufanya mazoezi
ya kujenga mwili na kusahau kuwa ni moja ya kuimarisha afya kuepuka magonjwa yakiwemo presha na mafuta
mwilini----tubadilikeni ulimwengu huu ulioacha vyakula vya asili” alisema
Mtulya
Aliitaka jamii kujipenda kwa kufanya
mazoezi na kupima afya zao kila baada ya muda jambo ambalo litaifanya miili yao
kuwa imara na kuepuka magonjwa ya mara kwa mara.
No comments:
Post a Comment