Saturday, May 23, 2015

WANAOTAKA NDOA YA JINSIA MOJA (USHWETWANI) WAELEKEA KUSHINDA

Wanaopinga ndoa za jinsia moja wasalimu

Wapiga kura wa Ireland
Huku kura zikiendelea kuhesabiwa baada ya kura ya maoni nchini Ireland kuhusu uhalalishaji wa ndoa za jinsia moja,kiongozi mmoja anayeongoza kampeni za kupinga ndoa hizo amekubali kushindwa.
David Quinn,kiongozi wa taasii moja  inayokuza dini katika jamii ,aliwapongeza wanaotaka sheria kubadilishwa.
Matokeo rasmi yanatarajiwa kutolewa baadaye jioni hii.
Iwapo mabadiliko hayo yataidhinishwa ,Ireland itakuwa nchi ya kwanza kuruhusu ndoa za jinsia moja kupitia wingi wa kura.

No comments:

Post a Comment