Tuesday, May 26, 2015

ULAJI WA NYAMA NYEKUNDU NA MAFUTA HATARI YA SARATANI YA UTUMBO

Utafiti:Uzito mkubwa ni hatari

Watafiti wanasema kuwa matumizi makubwa ya Nyama nyekundu na Mafuta kwa wingi ni hatari kwa Afya
Kuwa na uzito mkubwa katika umri mdogo kunaweza kusababisha ugonjwa wa saratani ya utumbo hapo baadae
Watafiti walikuwa wakiwafuatilia wanaume takriban 240,000, Raia wa Sweden kwa miaka 35.
Uchambuzi uliochapishwa kwenye jarida moja, unaonyesha kuwa vijana wadogo walikuwa hatarini mara mbili zaidi kupata maradhi ya Saratani ya utumbo, takwimu zilikuwa juu zaidi kwa vijana wadogo wenye uzito mkubwa .
Shirika la kimataifa la utafiti wa Saratani limesema uhusiano kati ya uzito mkubwa na saratani una “nguvu”.
Saratani ya utumbo ni aina ya saratani ya tatu ambayo huwakumba walio wengi duniani, ikiripotiwa kugunduliwa kwa wagonjwa milioni 1.4 kila mwaka.
Ulaji wa Nyama nyekundu na matumizi ya Mafuta kupita kiasi husababisha uzito mkubwa.
Waliojitolea kwenye utafiti huo walikuwa na umri wa kati ya miaka 16 na 20 kwa kuanzia.wengi wao walikuwa na uzito wa kawaida,
Rachel Thomson ni mtafiti kutoka Shirika la kimataifa la utafiti wa Saratani,amesema kuwa uzito wa kupita kiasi unaweza kusababisha Kansa ya utumbo
Hutopitwa na habari inayonifikia na niko tayari kukusogezea hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment