Tuesday, May 26, 2015

AOTA KUMUOA BINTI WA RAIS

Wakili wa Kenya na ndoto za kumuoa mtoto wa Rais wa Marekani..

President Barack Obama is greeted by daughter Malia as he arrives for the 57th Presidential Inauguration ceremonial swearing-in at the US Capitol on January 21, 2013 in Washington, DC. AFP PHOTO/Jewel Samad        (Photo credit should read JEWEL SAMAD/AFP/Getty Images)
Kuna baadhi ya wanaume wana ndoto siku moja wawe na uwezo wa kumuoa mtoto wa Rais wa Marekani aitwaye Malia Obama, lakini swali je ni kweli itawezekana?.
Mmoja mwenye ndoto kama hiyo ni wakili kutoka Kenya ambaye amesema atajitoa kwa kila hali kuhakikisha anatimiza ndoto zake za kuweza kumpata mtoto huyo huku akimuahidi Rais Barack Obama vitu mbalimbali kama mahari kwake.
wakili
Kiprono Matagei amesema yupo tayari kumzawadia rais huyo ng’ombe 50, kondoo 70 na mbuzi 30 ili ampe mtoto wake Malia ambaye kwa sasa ana miaka 17.
Amesema alianza kumpenda mtoto huyo tangu mwaka 2008 wakati akiwa na miaka 10 na alikua akisubiri apate nafasi hiyo, na sasa anatumia mwanya wa Rais huyo atakapofanya ziara nchini humo mwezi ujao ili aweze kuongea naye.
Amesema familia yake imeridhia kumsaidia kufanikisha kumpata mtoto huyo kwa kuchangia gharama za mahari aliyoahidi kumpa Rais huyo.
Kwa habari na matukio kemkem usiwe mbali namio nia hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment