Sunday, May 31, 2015

MAFURIKO MIKANJUNI ,TANGA

Zaidi ya falimia 11 mtaa wa Mikanjuni A kata ya Mabawa Tanga hazina mahala pa kuishi baada ya nyumba zao kuzingirwa  na maji baada ya mvua iliyonyesha kwa siku mbili mfululizo.
Kujaa kwa maji hayo pia imedaiwa kusababishwa na kutokuwepo kwa miundombinu ya kupitisha maji na hivyo kuwa sababu ya maji kuingia majumbani.
Wakizungumza na tangakumekuchablog mapema leo, wakazi hao walisema kwa muda mrefu wamekuwa wakiwaeleza viongozi juu ya kero hiyo lakini hakuna jitihada zozote zinazochukuliwa.

 Wakazi wa mtaa wa  Mikanjuni A kata ya Mabawa Tanga, wakiangalia nyumba iliyozingirwa na maji baada ya mvua kubwa kunyesha kwa siku mbili mfululizo ambapo jumla ya familia 11 hazina pahala pakuishi. Maji hayo hayana njia za kupita baada ya kutokuwepo kwa miundombinu ya mifereji ya kupitisha maji.


Kwa habari, matukio na burudani ni hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment