Thursday, May 28, 2015

POWER BANK YAUWA MTU

Power bank imesababisha kifo kwa binti huyu, unajua ilikuaje..?

power
Matumizi ya simu za Smartphone yamezidi kuongezeka siku hadi siku na sasa kumekuwepo na urahisishaji wa matumizi hayo baada ya kuonekena kutumika muda wote, kumekuwepo na teknolojia mpya inayosaidia kuchaji simu hizo,.
Kutokana na simu hizo kuwa busy muda wote, kuna kifaa cha powerbank ambacho kinarahisisha matumizi yake kwa kuchaji simu muda wowote na mahali popote.
Kuna Stori imetokea huko Hgana leo ambayo  inamuhusu msichana mmoja ambaye amefariki dunia wakati akiichaji powerbank yake.
Msichana huyo aitwaye Blandine alikua akichaji simu yake wakati akiwa anachat na marafiki zake huku akiwa amechomeka powerbank yake.
Baada ya muda aliishiwa na usingizi huku akiwa ameweka powerbank kwenye socketi wakati umeme ukiwa umekatika kwa madhumuni ukirudi uingie moja kwa moja.
Lakini baada ya umeme kurudi, powerbank hiyo ilipata moto na kungangania mwilini mwake ambapo ilipelekea kupoteza maisha na taarifa hiyo ilitolewa na wazazi wake waliogundua  kifo chake.

No comments:

Post a Comment