Friday, May 29, 2015

SHIRIKA LA MADINI LA TAIFA (STAMICO) LAANZA UTAFITI WA GESI ASILIA MKINGA, TANGA

 Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeshinda ukandarasi uchorongaji wa miamba kutoka shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC)  kwa hatua za awali kubaini uwepo wa Gesi Asilia na mafuta kijiji cha Jirihini kata ya Gombero Wilayani Mkinga Mkoani Tanga.
Jumla ya mita  1,500 zinatarajiwa kuchorongwa na wataalamu wa Uchorongaji wa STAMICO ndani ya siku 45 kwa mashimo 10.

Jumla ya mashimo 10 yanatariwa kuchorongwa yenye wastani wa urefu wa mita 150 kila moja na kutumia utaalamu aina ya Diamond ambao hutoa sampuli ya mwamba halisi bila kuupondaponda.

Baaadhi ya wakazi kijiji cha Jirihini wameichukulia hatua hiyo kama ukombozi kuelekea maisha bora kila Mtanzania kwa madai kuwepo kwa Gesi na mafuta kijijini hapo kutayabadilisha maisha yao pamoja na wakazi wa Mkoa wa Tanga jumla.

Hii imeleta faraja hata kwa baadhi ya Wilaya jirani na Mkoa kwa jumla kwani wamedai kuwepo kwa Gesi na mafuta hali za wananchi zitabadilika na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa kampuni hiyo ya uchimbaji na wataalamu wake ili utafiti ubaini kuwepo kwa Gesi .kijijini hapo.












No comments:

Post a Comment