Saturday, May 23, 2015

BENITES KUMRISI ANCELOTTI

Real Madrid yawasiliana na Benitez

Rafael Benitez
Mkufunzi wa kilabu ya Napoli Rafael Benitez ameorodheshwa miongoni mwa makocha wataokumrithi Carlo Ancelotti katika kilabu ya Real Madrid.
Ancelotti anatarajiwa  kuachana na kilabu hiyo baada ya mechi ya mwisho na Getafe wikiendi hii.
Mazungumzo kati ya Real Madrid na Benitez yanaendelea huku  Benitez katika kilabu ya Napoli ikitarajiwa kukamilika mwezi ujao,ijapokuwa hakuna makubaliano yalioafikiwa.
Klabu ya West Ham pia iliwasiliana na kocha huyo ambaye aliwahi kuifundisha  Chelsea na Liverpool.

No comments:

Post a Comment