
Amini usiamini huku
watu wengi Afrika Mashariki wakilazimika kulipa mabilioni ya shilingi
ilikujifunza kuendesha magari,teknolojia sasa imepiga hatua moja zaidi.
Mwanzo
ilikuwa ni magari madogo sasa kampuni ya kutengeneza magari ya kifahari
Daimler Mercedes-Benz imezindua lori linalojiendesha lenyewe!Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo yenye asili yake nchini Ujerumani,Wolfgang Bernhard alibofya kitufye na mara lori likachukua usukani na kuenda lenyewe pasi na kusababisha ajali ya aina yeyote.
.
Aidha mtambo huo unatumia na kupokea taarifa na mawasiliano iwapo lori hilo linasogea karibu zaidi kitu chochote iwe ni gari,mti ama hata mtu barabarani.
Hata hivyo kampuni hiyo ilisisitiza kuwa sharti dereva awe hapo wakati wote kifaa hicho cha "highway pilot" kinapotumika kama tahadhari kusitokee ajali.
.
Kwa mujibu wa bwana Bernhard lori hilo lilimudu kujiendesha na hata kutimia kasi ya Kilomita 80 kwa saa.
.
Bernh
ard
alissistiza kuwa wakati dereva anapohisi amechoka gari hilo linaweza
kuchukua usukani naye ajipumzishe kidogo japo kwa kutengeneza kikombe
cha chai huku kamera na mfumo huo wa radar zikidhibiti usukani.''Kwa hakika hata uwe mstadi kivipi , mfumo huu wa "highway pilot" unaendesha vyema zaidi kuliko mwanadamu na hata iwe kwa kiwango kipi haiwezi kuchoka sawa na vile madereva wa malori huwa wanawachoka na kupoteza umakinifu barabarani.'' alisema mkurugenzi wa kampuni hiyo Wolfgang Bernhard
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment