Mmea unaokula wadudu

Mmea unaokula wadudu unatumia nguvu za matone ya mvua ili kuwakamata wadudu hao,wanasayansi wamebaini.
Wanasayansi
hao kutoka chuo kikuu cha Bristol wamebaini kwamba matone hayo ya mvua
husababisha mtikisiko katika majani ya mti huo ambayo yana umbo la
mtungi.Hatua hiyo huwapeleka wadudu katika mfuniko wa mtungi huo wenye mtego, ambapo wadudu hao huzamishwa na kuliwa.
Matokeo ya utafiti huo yaliochapishwa katika jarida la PNAS yanatokana na kamera zenye kasi na zisizo
na mtikisiko mkubwa.Hatua hiyo ni ya kipekee miongoni mwa mimiea , Daktari Bauer anasema.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment