Haya ni maamuzi ya Man United ambayo yalimkera Patrice Evra …
         
Beki wa kimataifa wa Ufaransa Patrice Evra ambaye amewahi kuitumikia klabu ya Manchester United ya Uingereza kwa kipindi cha miaka nane, October 14 amezungumzia uamuzi wa Man United kumuacha aondoke timu hiyo na kutimkia klabu ya Juventus ya Italia.
Patrice Evra ambaye amedumu katika klabu ya Manchester United kwa kipindi cha miaka nane, hakufurahishwa na uamuzi wa Man United kumuuza kwenda Juventus ya Italia kwa dau la pound milioni 1.5. Licha ya kushinda mataji kadhaa akiwa katika klabu yake mpya ya Juventus, Evra anasema uhamisho wa yeye kuondoka Man United ulilazimishwa na wala haukuwa uamuzi wake.

“Bado 
ni ngumu kuzungumzia kuondoka kwangu Man United lakini siku moja 
nitakapokuwa nimestaafu soka nitakuwa tayari kuzungumzia hili kwa kina. 
Nilikuja Turin kwa ajili ya familia yangu sababu Man United waliingiza 
kifungu ambacho kilibadili kila kitu, kitu ambacho 
kilinikera”>>> Evra
“Lakini
 sijutii uhamisho huu ambao mwisho wake umekuja kuwa na mrejesho zaidi 
ya chanya kwangu, najisikia furaha Serie A licha ya kuwa uhamisho huu 
ulikuwa wa bahati mbaya kuliko chaguo langu. Kwa sasa malengo yangu ni 
kuhakikisha nashinda mataji Juventus na timu yangu ya taifa ya 
Ufaransa”>>> Evra

Beki huyo wa zamani wa klabu ya Manchester United ya Uingereza, akiwa na Man United amecheza jumla ya mechi 379 na kutwaa mataji matano ya Ligi Kuu Uingereza, moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya na mataji mengine tisa hiyo ni kwa muda wa miaka nane aliyodumu katika klabu hiyo.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment