Kuanzia sasa hivi, wakali wa Arsenal ni mwendo wa suti tu wanapoingia uwanjani..!!
         
Klabu ya Arsenal ya Uingereza ambayo inafundishwa na kocha raia wa Ufaransa Arsene Wenger,
 October 14 wachezaji wa timu hiyo wameingia kwenye headlines za 
mitandao ya kijamii baada ya kuonekana wamevaa suti huku wakioneshana 
ufundi wa kuchezea mpira.
Suti hizo nyeusi ambazo wamevaa 
wachezaji hao zinaonekana kuwa za kufanana na kwa haraka ukiwaona 
utatamani ujue kuna sherehe inayofanya nyota hao kuvaa suti 
zinazofanana? Ripoti kutoka mirror.co.uk inasema kampuni ya nguo za kiume ya Duchamp London imeidhamini klabu ya Arsenal.
Duchamp London ambayo inajihusisha na utengenezaji wa suti hizo inatajwa kuingia mkataba na Arsenal, hivyo itakuwa inawavalisha wachezaji wa Arsenal,
 makocha na viongozi wa klabu hiyo wakiwa katika mechi au katika sherehe
 mbalimbali zitakazokuwa zinahusisha wachezaji na viongozi wa klabu 
hiyo.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog 





No comments:
Post a Comment