Wizi kutokea eneo la ajali sio kwa Bongo pekeyake, imemkuta na huyu mama Marekani..
Kwenye matukio ya ajali wizi nao huwa
unakuwepo, yani mfano imetokea ajali wapo wanaokuja kwa lengo la
kusaidia majeruhi wa ajali, lakini wapo wanaokuja na malengo na maslahi
yao mengine kabisa tena bila hata kutoa msaada wowote !!
Ripoti za wizi kwenye ajali sio stori
ngeni kwenye maeneo mengi ya nchi kama Tanzania, umewahi kuhisi kwamba
hata Ulaya na Marekani hiyo kitu ipo?
Taarifa ikufikie kwamba imemkuta mama mmoja wa Kimarekani, Kimberly Smith ambaye alipata ajali na gari lake maeneo ya Irving, Texas Marekani… gari ilipinduka mara tatu nje ya barabara
Mtu wa kwanza kufika eneo hilo alikuwa
jamaa mmoja aliyesimamisha gari akajifanya kama anataka kutoa msaada kwa
mama huyo kwa sababu alikuwa na majeraha na alikuwa amenasa ndani ya
gari.
Badala ya kutoa msaada, huyo jamaa alimnyang’anya Kimberly
pochi yake na kuingia kwenye gari yake, alafu akaondoka zake !! Baada
ya muda kidogo akatokea msamaria mwingine ambaye alimsaidia mama huyo na
kupiga simu ya dharura Polisi na Hospitali kwa ajili ya kumsaidia mama
huyo.
No comments:
Post a Comment