Pale ambapo viatu vimesababisha Mwanariadha wa Kenya ashindwe kuvunja Rekodi ya Dunia..
Eliud Kipchoge
ni Mwanariadha aliyewakilisha Kenya kwenye Mashindano ya Riadha ya
Berlin Marathon ambayo yamefanyika Berlin Ujerumani… Round ya kwanza
haikuwa na neema kwake, ulimi wa ndani ya viatu ulitoka na kusababisha
jamaa ashindwe kuivunja Rekodi ya Dunia kwenye Mashindano hayo.,
Unaweza kuchukulia ni kitu cha kawaida, lakini Eliud anasema
mpaka anamaliza mbio alikuwa na malengelenge miguuni pamoja na kidole
gumba kupata jeraha na kutokwa damu nyingi, hiyo ilifanya amalize round
zote za Riadha akiwa na wakati mgumu sana !!
“Haikuwa
siku nzuri mimi kutumia hivi viatu, nilivijaribu nikiwa Kenya na
vilikuwa sawa tu!! Lengo langu ilikuwa nivunje Rekodi ya Dunia leo
lakini naona haikuwa siku yangu”– Eliud Kipchoge.
Mbali ya changamoto zote, Eliud aliibuka na ushindi kwenye mbio za Maili kumi huku akiweka Rekodi ya kumaliza mbio kwa saa mbili na dakika nne.
Unaweza kucheki kwenye hii video ya sekunde 76 mbio zenyewe ilivyokuwa mpaka mwisho…
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment