Monday, July 25, 2016

KOLO TUURE ATIMKIA CELTIC

Kolo Toure ajiunga na klabu ya Celtic

Mchezaji mpya wa klabu ya Celtic Kolo Toure anatumai kufanya vyema zaidi katika timu yake mpya hususan baada ya kukutanishwa tena na aliyekuwa mkufunzi wake Brendan Rodgers.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 35 alifanya kazi na Rodgers akiwa Liverpool.
''Ni Meneja mzuri kwangu, yeye ni mmoja wa makocha bora'', alisema raia huyo wa Ivory Coast.
''Alifanya kazi nzuri akiwa Swansea na baadaye akaajiriwa Liverpool ambapo alifanya vyema na natumai atafanya vizuri hapa'',aliongezea.
Baada ya kusaini kandarasi ya mwaka mmoja,Toure ambaye ameichezea Arsenal na Manchester City hatashirikishwa katika mechi ya kwanza ya vilabu bingwa huko Kazakhstan.
''Niko tayari lakini kwa sababu ndio nimejiunga na timu hii, nahitaji muda kuwa tayari''.

No comments:

Post a Comment