Ufaransa kupinga ufadhili wa nje wa misikiti
Waziri mkuu wa
Ufaransa Manuel Valls amesema kuwa huenda akapendekeza kupigwa marufuku
kwa muda ufadhili wa misikiti kutoka nje kufuatia mashambulio ya hivi
karibuni yanayotekelezwa na wana jihad.
Akizungumza na gazeti la
Le Monde ,bwana Valls pia amewataka maimamu wote wa Ufaransa kupewa
mafunzo ndani ya Ufaransa na wala sio nje ya taifa hilo.Amesema ni wakati ambapo Ufaransa inafaa kujenga uhusiano mpya na Islam,akitaja vita dhidi ya itikadi kali kama jukumu la kizazi hiki.
Serikali ya Ufaransa imekosolewa kwa kushindwa kuzuia mashambulizi matatu katika kipindi cha miezi 18 iliopita.
No comments:
Post a Comment