Bill Clinton: "Rafiki yangu" Hillary anafaa kuwa rais

Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton amemsifu sana mkewe Hillary na kusema anafaa kuongoza taifa hilo.Kwenye hotuba yenye hisia kali, amemweleza Hillary kama “rafiki mkubwa” na akasimulia walivyokutana na jinsi anavyojitolea katika utumishi wa umma.
Saa chache awali, mkewe aliibuka kuwa mwanamke wa kwanza nchini Marekani kuidhinishwa kuwania urais na chama kikubwa
Bi Clinton alihitimisha shughuli za usiku huo wa Jumanne kwa ujumbe wa video.
No comments:
Post a Comment