CAF yapata mdhamini mpya
Shirikisho la Soka
barani Africa (CAF) limepata mdhamini mpya baada ya kumalizika kwa
mkataba wake na kampuni ya mawasiliano ya Orange.
Orange imekuwa mdhamini mkuu wa mashindano makubwa ya CAF kwa miaka minane tangu 2009.Kabla ya hapo, kampuni nyingine ya mawasiliano ya MTN ndiyo iliyokuwa mdhamini kwa miaka minne.
Sasa, mdhamini mpya atakuwa kampuni ya mafuta na gesi ya Total kutoka Ufaransa.
Kampuni hiyo itaanza kwa kudhamini michuano ya Kombe la Taifa Bingwa Afrika mwaka 2017 ambayo itaandaliwa nchini Gabon.
Thamani ya mkataba huo haijafichuliwa.
Total itakuwa mdhamini mkuu wa:
- Kombe la Taifa Bingwa Afrika
- Ligi ya Klabu Bingwa Afrika
- Kombe la Taifa Bingwa Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN)
- Super Cup ya Afrika
- Kombe la Mashirikisho
- Kombe la Taifa Bingwa Afrika kwa Wanawake
- Kombe la Futsal Afrika
- Kombe la Taifa Bingwa Afrika wachezaji wa chini ya miaka 23
- Kombe la Taifa Bingwa Afrika wachezaji wa chini ya miaka 20
- Kombe la Taifa Bingwa Afrika wachezaji wa chini ya miaka 17
No comments:
Post a Comment