Bilionea mtanzania katoa sababu za kwanini hajanunua ndege binafsi
Kama ni msomaji na mtumiaji mzuri wa
mitandao hususani ya kijamii, basi utakuwa ushawahi kukutana na
headlines za mtanzania katika jarida la Forbes, mtanzania Mohammed Dewji ambaye amewahi kutajwa na Forbes kama bilionea wa 24 barani Afrika, amefunguka na kueleza sababu za yeye kutonunua ndege binafsi licha ya kuwa bilionea.
“Nimefanya
Interview na Forbes wakaniuliza kwa nini sijanunua ndege binafsi,
wakati bilioni 10 au 20 unapata ndege, mimi nimepiga mahesabu nikikata
tiketi ya daraja la kwanza kwenda Afrika Kusini kwenda na kurudi natumia
milioni 4, ila kwa ndege binafsi ikiruka angani saa moja gharama yake
milioni 8”
millardayo
No comments:
Post a Comment