Friday, July 29, 2016

MSIMU WA MIHOGO NA VIAZI TANGA

 Wafanyabiashara wa mihogo na viazi Soko la Mgandini Tanga, wakipanga kusubiri watja sokoni hap kama walivyokutwa na Camera za Tangakumekucha, Msimu huu wa viazi na mihogo umetajwa kuwa wakulima wa mazao hayo wanaendelea kuvuna kwa wingi hii ikiwa ni kutokana namvua kunyesha kwa wingi sehemu mbalimbali za Mkoa wa Tanga.
Hata hivyo wafanyabiashara na wakulima hao wamelalamikia uhaba wa soko hivyo viazi na mihogo yao kuuza kwa bei ya hasara ili kuepuka kuwaozea mikononi.
Wafanyabashara hao na wakulima wameiambia Tangakumekucha kuwa kama Serikali itajenga kiwanda cha kusindika matunda na mihogo kilimo chao kinaweza kuwa na tija na kuwa mfano kwa wengine ambao mashamba yao wameyatekeleza kwa kuona kilimo hicho hakina tija.




Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment