jamaa anayewatoa mabinti wa kike usichana Malawi imeifikia Serikali
Raia
mmoja wa Malawi alionekana katika habari moja ya BBC akihusishwa na
tambiko la usafishaji wa wasichana wadogo kupitia kushiriki ngono nao
amekamatwa.
Eric Aniva
amekamatwa kufuatia agizo la Rais Peter Mutharika kulingana na
mkurugenzi wa mawasiliano ikulu ya Rais, Bright Molande aliyezungumza na
BBC, Molande amesema kuwa kutokana na uovu huo Aniva atashtakiwa kwa
kukiuka haki za watoto.
Aidha
aliongeza kuwa Rais amechukizwa na yaliofichuliwa katika habari hiyo na
ameapa kukabiliana na tamaduni hiyo. Mtu aliyetajwa katika habari hiyo
ambaye alifanya mapenzi na zaidi ya wasichana 100 pia imebainika kuwa
alikuwa na virusi vya ugonjwa wa UKIMWI.
Source; BBC
No comments:
Post a Comment