Ndege aliyesafiri kutoka Finland hadi Uganda


Ndege mmoja ambaye inaaminika alitoka nchini Finland amepatikana katika uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda.Isaac Mujaasi, afisa wa mauzo na mawasiliano katika UWEC, ameambia BBC kwamba ndege huyo alikuwa ameumia katika mabawa yake baada ya kugongwa na ndege iliyokuwa inapaa.
Bw Mujaasi anasema waliwasiliana na maafisa wa makumbusho hao ambao wamethibitisha kwamba ndege huyo ni wao.
Afisa huyo hata hivyo amesema ni kawaida kwa ndege kuhama kutoka Ulaya, hasa wakati wa majira ya baridi na kukimbilia maeneo yenye joto.
No comments:
Post a Comment