Sunday, July 24, 2016

GUADRIOLA ASMA HANA BIFU NA MOURINHO

Guardiola amesema atamsalimia Mourinho kwa mkono

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola, hatakuwa na tatizo lolote kumsalamia kwa mkono meneja wa Man U Jose Mourinho, wakat wa mechi kati ya vilabu hivyo mjini Beijing.
Mechi hiyo itakuwa ya pili kati yao tangu wote waache kufunza vilabu vya Barcelona na Real Madrid mwaka 2012.
Wote wamekana tofauti zoa na Guardiola anasme kuwa atamsalamia kwa mkono kama njia ya urafiki.
Wakati Mourinho naye aliulizwa kuhusu suala hilo, pia alisema kuwa atamsalamia Guardiola kwa mkono.
"Nilifanya kazi naye kwa miaka mitatu huko Barcelona, Tumesimamia tofauti, uhusiano kati yetu ni wa kawaida, alisema Mourinho.

No comments:

Post a Comment