Wednesday, July 20, 2016

BIASHARA KITUONI



Wafanyabiashara maarufu kama wamachinga kituo kikuu cha Mabasi yaendayo Mikoani cha Kange Tanga, wakitafuta wateja kupitia vifoo vya madirisha ya magari. Wafanyabiashara hao wamekuwa wakiendesha biashara yao na kutokuwa na sare za kuwatambulisha jambo ambalo limekuwa likiwakwaza wateja na abiria baada ya kutokuwa na utambulisho. Hii imekuwa ikijenga hofu ya uaminifu kituoni hapo kama alivyodai mmoja wa abiria ambaye alikuwa akienda Arusha , Pamela Chilongola.








No comments:

Post a Comment