Tuesday, July 26, 2016

MVUA YA SAMAKI, WAJIZOLEA MTU TANI YAKE, THAILAND

Mvua ya samaki ilivyotingisha Thailand

Hebu vuta picha, umeamka asubuhi na kuingia barabarani kwa ajili ya kuelekea eneo lako la kazi ghafla unakutana na samaki wengi wakiwa wametapakaa kwenye lami, huku watu wakieleza kwamba samaki hao wamedondoka kutoka angani kufuatia mvua kubwa iliyonyesha usiku!
Ni jambo la ajabu si ndiyo?


Basi kwa taarifa yako, tukio kama hilo limewahi kutokea nchini Thailand. Aprili 16, 2015, wananchi wa Thailand walishuhudia tukio la ajabu la maelfu ya samaki kukutwa barabarani, huku ikielezwa walishuka na mvua iliyonyesha usiku kucha.

Habari hiyo ilisambaa kwa kasi ikisindikizwa na picha zilizokuwa zinaonesha barabara ya lami ikiwa imefurika samaki hao.

Hata hivyo, baada ya taarifa hizo kuwa zimesambaa kwa kasi ya ajabu na kuzua mshangao karibu dunia nzima, baadaye ilibainika kwamba samaki hao hawakuwa wameshuka na mvua kutoka angani.

Taarifa kutoka kwenye mamlaka zinazohusika, zilieleza kwamba samaki hao walitapakaa barabarani baada ya lori kubwa lililokuwa limebeba shehena ya samaki hao, likielekea kwenye Mji wa Guizhou Kaili, kupata hitilafu kwenye milango yake.

Taarifa ilieleza kwamba mlango wa nyuma ulifunguka bila dereva kujua, samaki wakawa wanadondoka barabarani kwa wingi ndipo watu wakazusha kwamba waliletwa na mvua kubwa iliyonyesha usiku,” ilikaririwa taarifa kutoka kwenye mamlaka zinazohusika nchini humo na kumaliza utata kuhusu ‘mvua ya samaki’.

No comments:

Post a Comment