Wanawe Trump wafana kongamano la Republican
Wana wawili wa
mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump ni
miongoni mwa watu waliohutubu katika kongamano la kitaifa la chama hicho
mjini Cleveland, Ohio.
Kinyume na mkewe Trump, Melania, ambaye
alishutumiwa sana alipotoa hotuba siku ya kwanza baada ya kubainika
kwamba baadhi ya maneno kwenye hotuba yake yalitoka kwenye hotuba
iliyotolewa na mke wa Rais Barack Obama, Michelle, mwaka 2008, wawili
hao walisifiwa sana.Mwanawe wa kiume, ndiye aliyetangaza kwamba babake alikuwa amepata wajumbe wa kutosha na kuidhinishwa kuwa mgombea rasmi wa chama hicho.
No comments:
Post a Comment